Tuesday, February 14, 2012

MKOTA NA JUHUDI WAWAKILISHA PEMBA KTK BUSARA

Kundi la Juhudi Taarab la Chake-Chake wakitumbuiza ktk Sauti za Busara

Mkota Spirit Dancers wakitawala jukwaa siku ya ufungzi wa Busara 2012

Bosso la chambi laivu ndani ya Ngome Kongwe kutoka kwa Mkota
Wiki iliyopita Swahili Center ilifanikiwa kutimiza azma yake ya kuongeza uwakilishi wa sanaa za Zanzibar katika matamasha yanayofanyika Zanzibar kwa kuvileta vikundi viwili kutoka Pemba. Vikundi vilivyowakilisha sanaa za maonesho za asili za Zanzibar katika tamasha la Sauti za Busara la 2012 ni Mkota Spirit Dancers kutoka Mkoani na Juhudi Taarab kutoka Chake-Chake.

Uwakilishi wa vikundi hivyo kupitia Swahili Center umewezeshwa kwa ufadhili wa kampuni ya safari za anga ya hapa Zanzibar, ZanAir Ltd, ambayo mwaka huu inasherehekea miaka 20 ya utaoji huduma tangu kuanzishwa 1992

Katika tamasha hilo, kundi la Mkota Spirit Dancers waliwatangulia Juhudi Taarab kwa kufanya oehso lao tarehe 9 February katika ukumbi wa Mambo Club, ndani ya Ngome Kongwe. Wakiwa wamepangiwa kutumbuiza katika siku hiyo ya ufunguzi, kundi hilo liliacha maji katika jukwaa kufuatia shoo yao ya ngoma ya Kumbwaya.

Juhudi Taarab nao walipata fursa ya kuonesha kilichowawezesha kuwepo katika 'gemu' kwa zaidi ya miaka 70 kwa kuja jukwaani siku ya Jumamosi tarehe 11 Februari na kuwalemaza wapenzi wa Taarab asilia kwavibao vyao kama vile 'Vijumbajumba' iliyiombwa na mtunzi wake Malik Hamad 'Wastara'. Isitoshe, mkali wa shairi la 'Bora Niombe', Ali Said 'Wazera' pia alikuwa jukwaani na kuimba 'Karamu' huku wapenzi wake wakiserebuka pembezoni mwa jukwaa.

Kwa ujumla, kuwepo kwa Mkota Spirit Dancers na Juhudi katika tamasha la mwaka huu la Sauti za Busara ni sehemu muhimu  katika kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa Swahili Center mwaka jana. Kutokana na hilo, ni matumaini yetu kuwa maonesho ya vikundi hivyo kutoka hapa nyumbani, yaliyokuwa na ubora wa hali ya juu, yameonekana na kuwa huenda ikiwa ndiyo mwanzo wa vikundi hivyo kupata ajira wanazostahili.

Swahili Center inapenda kutoa shukrani za dhati kwa kampuni ya ZanAir kwa ukarimu wake na kwa Busara Promotions kwa mashirikiano mazuri baina ya taasisi zetu.

Watendaji wa Swahili Center wakiwa na Mkurugenzi wa Busara, Yusuf Mahmoud

 
Mdau Salma Said akiwa na kundi la Mkota Ngoma (pembeni: Mahsin)
Watendaji wa Swahili Center wakiwa na kundi la Juhudi kufuatia onesho lao







Wednesday, January 25, 2012

SEARCH FOR COMMON GROUND WAITEMBELEA CENTER


Kutoka Kushoto: Bi Marks, Mahsin, Kheri na Bi Manirakiza

Watendaji kutoka taasisi ya Search for Common Ground yenye makaomakuu yake nchini Marekani, leo walitembelea ofisi ya Swahili Center katika jitihada za kuimarisha mahusiano baina ya asasi mbili hizo za kiraia.

Katika ujuio huo, taasisi ya Search for Common Ground iliwakilishwa na Bi Susan  Collin Marks ambaye ni Senior Vice President wa taasisi hiyo pamoja na Bi Spes Manirakiza ambaye ndiye atakayekuwa Mkrugenzi wa taasisi hiyo katika ofisi yao mpya iliyopo Zanzibar.
Wakati wa ziara hiyo ya kirafiki, wageni kutoka Search for Common Ground walipata fursa ya kupitia tathmini juu ya mradi wa 100% Zanzibari uliofanyika kuanzia mwezi wa Oktoba hadi Desemba 2011 kutoka kwa watendaji wa Swahili Center.
Akiwapokea wageni hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Swahili Center, Kheri Jumbe, aliwatambulisha mafanikio pamoja na changamoto zilizojiri katika utekelezaji wa mradi wa 100% Zanzibari uliokuwa na malengo ya kuimarisha misingi ya maridhiano na umoja wa kitaifa wa Zanzibar.  Search for Common Ground ni taasisi iliyojikita katika kuwezesha jamii tofauti ulimwenguni kufikia maafikiano ya kuleta amani endelevu.
Akipokea tathmini hiyo, Bi Susan Collin Marks alipongeza upeo na  juhudi za Swahili Center katika kubuni mradi wa 100% Zanzibari na kuutekeleza kwa ufanisi wa hali ya juu licha ya changamoto zilizojitokeza. Pia aliwataka watendaji wa taasisi hiyo kuendelea kutumia vyema jukwaa la sana za maonesho katika kujenga umoja na mshikamano baina ya wananchi wa Zanzibar mbali na malengo mengine ya kazi za taasisi hiyo changa.
“Ni jambo la kupigiwa mfano kutokana na mabadiliko yaliyopatikana Zanzibar katika kipindi kifupi cha maridhiano ya kisiasa yaliyoafiiwa nchini kwenu,’ alisema Bi Marks. ‘Kilichobaki sasa ni kuyazalisha matunda ya matumaini hayo mapya na kuyafanya yenye manufaa na kiuchumi na kijamii kwa waZanzibari.’
Kwa upande wa Bi Manirakiza, yeye aliwaahidi watendaji wa Swahili Center kuwa akiwa Mkrugenzi wa taasisi hiyo hapa Zanzibar atajitahidi kadiri ya uwezo wake katika kufanya kazi na Swahili Center pamoja na kuwashiriisha wasanii katika miradi ya Search for Common Ground nchini Tanzania.
Ujio wa Search for Common Ground katika ofisi ya Swahili Center ni marejeo ya ziara ya kirafiki iliyofanywa na Mkurugenzi wa Swahili Center mwaka jana katika ofisi za Search for Common Ground iliyopo mjini Washington DC, Marekani.

Search for Common Ground - www.sfcg.org


Wednesday, January 18, 2012

ZANAIR YAIPIGA JEKI SWAHILI CENTER KUSHIRIKI BUSARA

Watendaji wa Swahili Center, wakiwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya ZanAir Bw. Ashish Nagewadia (Kushoto) pamoja na Reservations Supervisor Asya Abdulla (Wa Pili kutoka Kulia)

Kituo cha Swahili Center kimeingia makubaliano ya mashirikiano na mdau wa sanaa nchini, Busara Promotions, utakaotoa fursa ya kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara la 2012 kwa njia maalum.

Makubaliano hayo yamelenga kuipa fursa Swahili Center kudhamini vikundi viwili vya sanaa kutoka kisiwani Pemba kutoa burdani katika tamasha hilo litakalofanyika kuanzia tarehe 8 hadi 12 Februari 2012. Katika makubaliano hayo, Swahili Center itashirikiana na kampuni ya ndege ya ZanAir katika kuviwezesha vikundi vya Mkota 'Spirit Dancers' na Juhudi Taarab kushiriki katika tamasha.

Mkurugenzi wa Sanaa wa Swahili Center, Mahsin Basalama, ambaye ndiye mtekelezaji na msimamizi mkuu wa miradi yote kwa upande wa ubunifu alikaribisha fursa hiyo kwa kusema kuwa kuvitangaza vikundi vinavyofanya sanaa zenye ubora wa hali ya juu ni mojawapo katika mikakati muhimu ya Swahili Center.

Mkurugenzi wa Sanaa wa Swahili Center, Mahsin Basalama (kushoto) akipokezana hati ya mashirikiano na Msaidizi Mkurugenzi wa Busara Promotions, Rosie Carter
Kwa upande wa ZanAir, Meneja wa Mauzo na Masoko, Ashish Nagewadia alisema kuwa ushiriki wao katika kuleta vikundi hivyo kutoka kisiwani Pemba ni njia mojawapo ya kampuni ya ZanAir kutoa shukrani kwa watu wa Pemba kwa kutumia huduma zao. Kampuni ya ZanAir inatimiza miaka 20 ya kutoa huduma za usafiri wa ndege tangu ilivyoanzishwa mwaka 1992.

Taarifa kamili kuhusu makubaliano hayo zitatolewa rasmi baada ya kukamilika mipango husika ikiwemo kutangazwa kwa mfadhili wa mashirikiano hayo.

ZANAIR LTD - CELEBRATING 20 YEARS OF SERVICE

Tuesday, January 10, 2012

Swahili Center yamtunikia Dr. Karume nishani ya ‘Shujaa wa Zanzibar’ ikiwa ni hatua ya mwisho ya 100% Zanzibari


Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe, Dk. Amani Karume akipokea nishani ya "Shujaa wa Zanzibar" kutoka kwa Mzee Hassan Nassor Moyo. Wakishuhudia makabidhiano hayo ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe, Mhe. Ismail Jussa (kulia) na Kheri Jumbe ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Swahili Center.
Rais Mstaafu Mhe. Dk. Karume akiwa na ujumbe ulimtembelea. Kutoka Kushoto ni Mahsin Basalama (Mkurugenzi wa Sanaa/ Swahili Center), Mhe. Ismail Jussa, Mzee Hassan Nassor Moyo, Kheri Jumbe na Abbas Kadhim (Mdau wa Swahili Center)

Kituo cha Sanaa za Maonesho za Waswahili (Swahili Performing Arts Center)
Zanzibar kimemtunukia Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Dr. Amani Karume,
nishani ya ‘Shujaa wa Zanzibar’ ikiwa ni hatua ya mwisho katika
kuadhimisha kufikiwa kwa maridhiano na hatimaye serikali ya umoja wa
kitaifa nchini Zanzibar.

Dr. Karume alikabidhiwa nishani hiyo na mwanasiasa mkongwe Mzee Hassan
Nassor Moyo  siku ya Ijumaa tarehe 23 Desemba 2011 katika hafla fupi
iliyofanyika nyumbani kwake huko Mbweni nje kidogo ya Mji Mkongwe.

Akiwasilisha risala yake katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Swahili
Performing Arts Center Kheri Jumbe alitoa shukrani kwa Dr. Karume kutokana
na jitihada zake katika kuleta amani ya kudumu nchini Zanzibar.

Jumbe alieleza kuwa, taasisi yake iliona umuhimu wa kuandaa sherehe za
maridhiano kupitia mradi wa sanaa uliopewa utambulisho wa 100%  Zanzibari
(Mzanzibari asilimia moja) ili kuwaenzi waasisi wa maridhiano hayo na
kueliimisha wananchi juu ya umuhimu wake.

“Kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Oktoba 4 hadi Desemba 3, tumekwenda
katika mikoa yote ya Zanzibar na kuwasilisha ujumbe juu ya umuhimu wa
kuimarisha misingi ya umoja na kuweka mbele uzalendo, ‘ alisema Jumbe.

Akikabidhi nishani hiyo kwa Rais mstaafu huyo, Mzee Hassan Nassor Moyo alirejea
wasia wake wakutaka viongozi wakuu wa Zanzibar kutowavumulia watendaji wa
serikali wanaovuruga maridhiano.

Katika kuipokea nishani hiyo, Dr. Karume aliwapongeza watendaji wa Swahili
Center pamoja na wasanii walioshirki katika mradi huo kwa juhudi zao
katika kuyaendeleza maridhiano kupitia sanaa zilizobeba ujumbe huo.

Nishani kama hiyo ya ‘shujaa wa Zanzibar’ alitunukiwa pia Makamo wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika kilele cha
sherehe za maridhiano huko uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba tarehe 3
Desemba 2011. 
 
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif akipokea nishani ya "Shujaa wa Zanzibar" katika kilele cha sherehe za 100% Zanzibari: Shangwe za Maridhiano na Umoja wa Kitaifa
Wengine waliohudhuria katika uwasilishwaji wa nishani hiyo kwa Dr. Karume
ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe Ismail Jussa pamoja na
Mkurugenzi wa Sanaa was Swahili Center, Mahsin Basalama.

Kupitia mradi wa 100% Zanzibari wasanii 130 kutoka vikundi 11 vya sanaa za
maonesho walishiriki katika kambi za kjenga umoja na kufanya maonesho
nchini kote.

Mradi wa 100% Zanzibari umedhaminiwa na Ubalozi wa Norway pamoja na
kampuni ya mawasiliano ya Zantel.

Monday, November 21, 2011

NADI IKHWAN SAFAA, JUHUDI TAARAB ZAITEKA KISONGE



Wananchi wakiwa wametulia wakikongwa nyoyo zao na wasanii.

MAONESHO ya Taarab kushangilia maridhiano ya kisiasa Zanzibar, juzi yalihamia katika Uwanja wa Kisonge, ambapo vikundi vya nadi Ikhwan Safaa na Juhudi kutoika Chake Chake, Pemba viliwapa uhondo mashabiki wengi waliojimwaga kiwanjani hapo.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Swahili Performing Arts, lilivutia wapenzi wengi kutokana na nyimbo murua zilizoporomoshwa na waimbaji magwiji wa vikundi hivyo.

kundi la Juhudi ambalo lilikuwa la kwanza kupanda jukwaani, lilimudu vyema kuzikonga nyoyo za wananchi kwa nyimbo zao tamu kama vile 'Yatima', 'Zimekwisha enzi zako', 'Mshikamano' na Bora niombe' uliowavutia wangi.

Bibie Saada Mohammed Akighani wimbo wa Njangu.

Nalo kundi la Nadi Ikhwan Safaa liliamsha hisia za hadhira iliyofurika uwanjani hapo, kwa nyimbo za 'Wadhanifu' ulioghaniwa na mkongwe Sihaba Juma, 'Njangu' (Saada Mohammed), 'Hakika nnakupenda' (Ally Massoud)

Vibao vingine vilivyowazingua wapenzi ni 'Naomba kwako bibie'(Sameer Basalama),'Namuenzi'(Faudhia Abdullah), ambazo ziliwaibua washabiki kila mara katika viti vyao na kuungana pamoja kuserebuka.

Aidha wasanii wa vikundi hivyo kwa pamoja waliimba wimbo wa kusisitiza kuuendeleza muafaka na maridhiano kati ya wananchi wa Zanzibar, ukiwemo wimbo wa 'Maridhiano' (Faudhia Abdullah).

'Usiyalaumu macho' Mr. Wazera aliwakuna wananchi.

Msanii wa siku nyingi Sihaba Juma, alirudi tena jukwaani kugani wimbo 'Nnazama', klabu Wazera hajaonesha majojo majojo yake katika wimbo 'Usijalaumu macho', na Saada Muhammed akahitimisha onesho hilo kwa kibao 'Leo tena'.
Tamasha hilo limepangwa kuendelea tena Jumamosi ijayo katika ukumbi wa Ngome Kongwe, ambapo kundi la ' Unguja All Stars Taarab' na kikundi cha ngoma za asili 'Mkota' kutoka Mkoani Pemba vitatoa burdani mwanana. 

Ma mia ya watu walirindima katika uwanja wa kisonge.

Monday, November 7, 2011

KUMBWAYA LAWAPAGAWISHA NUNGWI


MKOTA wakilimwaga kubwaya, kabla ya wapenzi kuanza kupagawa

Sherehe za maridhiano na umoja wa kitaifa zilizoandaliwa na taasisi ya Swahili Center zinaendelea kwa kasi ambapo kwa Ijumaa iliyopita, vikundi vya Nyota ya Umoja (Maigizo,Nungwi) na Mkota Ngoma (Mkoani, Pemba) vilirindima katika kijiji cha Nungwi, Unguja.
Katika onesho hilo ambalo lilifanyika katika Uwanja wa Skuli ya Nungwi, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, wapenzi wa fani za sanaa za maonesho kutoka sehemu mbali mabli waliliminika na kujimwaga katika burudani hizo zilizoanza saa 10 alasiri.
Kundi la Maigizo la Nyota ya Umoja, maarufu kwa michezo yao kama vile ‘Dhulma Kafara’ na ‘Masikini naye Mtu’, walitoa burudani safi kupitia mchezo wa ‘Mchelea Mwana Kulia’ uliobeba maudhui ya umuhimu wa ushirikiano wa kuyalinda maadili ya KiZanzibari ndani ya jamii.
Nalo kundi la Mkota Ngoma kutoka Mkoani, walikonga nyoyo za wapenzi wa Ngoma na asili kwa kupiga ngoma zao za Msembwe, Unjunguu na Kumbwaya. Wengi waliohudhiria shehere hizo walivutiwa sana na umahiri wa kundi hilo katika kuzicheza Ngoma hizo.
Katika kuutambulisha mradi huo kwa waliohudhuria onesho hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Swahili Center Bw. Kheri Abdalla Yussuf, aliwajulisha wapenzi hao wa sanaa za utamaduni kuwa dhamira ya mradi huo ni kuimarisha misingi ya umoja wa kitaifa nchini Zanzibar kupitia sanaa za utamaduni zenye burudani na mafunzo kwa jamii yote.
Wakati huo huo, aliyekuwa mgeni rasmi katika onesho hilo, Mhe. Bi Riziki Juma Simai (Mkuu wa Wilaya ya Kasakazi A) aliwataka wananchi wa Nungwi na wote waliohudhuria kuimarisha misingi ya umoja wa kitaifa kwa vitendo.
Mradi wa 100% Zanzibari (tafsiri; Mzanzibari asilimia mia moja) umekuwa ukifanya maonesho katika Mikoa ya Unguja na Pemba kufuatia kambi za kisanii zinazoshirikisha fani za Taarab, Ngoma za Utamaduni na michezo ya Kuigiza. Shangwe hizo zimekuwa zikifanyika kwa awamu katika sehemu mbali mbali ambapo kwa kipindi cha Nov 15-19 zitahamia katika Mkoa wa Mjini Maghribi.
Swahili Performing Arts Center (Kituo cha Sanaa za Maonesho cha Waswahili) ni taasisi ya iliyoanzishwa kwa dhamira ya kuchangia katika maendeleo ya sanaa za maonesho asilia za Zanzibar pamoja na zile za mwambao wa Waswahili kupitia uwezeshaji (wasanii), uzalishaji wa kazi za sanaa, maonesho na ushirikishaji jamii. Dira ya Swahili Center ni kuurejeshea hadhi utambulisho wa utamaduni wa Kiswahili.
Mradi wa 100% Zanzibari umedhaminiwa na Ubalozi wa Norway pamoja na kampuni ya mawasiliano ya Zantel.

Sunday, November 6, 2011

SWAHILI CENTER REPRESENTS CULTURE STAKEHOLDERS IN GHANA FORUM



Mkurgenzi wa Swahili Center, Kheri Jumbe (wa pili kutoka kulia) akiwa na Meya wa Jiji la Accrapamoja na wajumbe kutoka nchi za Nigeria, Ghana, Angola, Ghana, Afrika Kusini, Moroko na Senegal.

During the week of November 7-10, the Zanzibar-based Swahili Performing Arts Centre Managing Director, Kheiri Jumbe, attended the African Cultural Capital’s City Forum on Culture and Development, in Accra, Ghana.

The Isles was invited on merit of both the tangible and intangible cultural assets present in Stonetown. In a telephone conversation on Friday, Jumbe told the ‘Daily News on Saturday,’ “I am here to attend a forum on strategies towards making culturally active African cities to be recognised by UNESCO as being that.” According to Jumbe the aim of the meeting was to strategise on ways to infuse culture and the creative industries agendas at the heart of national development policy.

Cultural leaders from several African countries got the chance to explore development policies in their respective countries in relation to funding modalities and programming approaches. Countries represented at the forum, which took place between Monday and Thursday this week were Cameroun, Morocco, South Africa, Nigeria, Mozambique, the hosts Ghana and Tanzania.


Kheri akitoa mada kuhusu ustawi wa sanaa na utamaduni wa Zanzibar ka mtazamo wa Swahili Center

The Mayor of Accra, Alfred Oko Vanderpuije, was the host of the 4-day event, which was organised by the City of Accra, The Arterial Network, UNESCO, The Goethe Institut and Agenda 21 of Spain. “My personal ambition and that of the Swahili Centre as stakeholders in culture in Tanzania is to develop ways in which the competitiveness of culture in the context of its productivity can be enhanced for the benefit of the local economy,” Jumbe replied when asked about the purpose of his participation.

He further explained that many studies conducted on the social and economic impact of cultural and creative industries have shown “positive contribution towards social cohesion, economic development and poverty reduction.” UNCTAD data shows that cultural and creative industries worldwide grew an average of 8.7 per cent annually.

However, Jumbe contended in many developing countries culture is not mainstreamed into development policies, despite “UNESCO recognising it as a vector for development and promoter of international co-operation.” As a result, there is generally lack of long-term, co-ordinated effort and funding in the sector in many developing countries. Inevitably, most support for culture in developing countries comes from international donors and multinational corporations, he maintained.

Kheri na mwenyeji wake Philibert wakitembelea kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Ghana Marehemu Kwame Mkrumah

These only tend to concentrate on short-term and highly visible projects that are usually insufficient to render the sector viable.